VUNJA VIFUNGO
JINSI YA KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA GIZA Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Leo tunajifunza jinsi ya kutoka katika vifungo vya kishetani. Kifungo cha kipepo ni nini? Kifungo cha kipepo ni adhabu ya mtu kuwekwa jela kipepo na mawakala wa shetani. Jela ni mahali wanapowekwa waharifu ili watumikie adhabu. Wako watu wengi tu wanateswa na vifungo vya giza katika maisha yao, wengine wanatamani watoke katika vifungo hivyo lakini imeshindikana maana hawaijui njia sahihi ya kuwatoa katika vifungo.. Jambo la kwanza kabisa nataka kukuambia ni kwamba Bwana YESU alikuja ili kuzivunja na kuziharibu kazi zote za shetani vikiwemo vifungo vya kipepo. 1 Yohana 3:8b ''Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. '' Kuna mambo mengi yanaweza yakahitajika ili hadi mtu husika afunguliwe kutoka vifungo vya giza. Kufunguliwa vifungo kunahitaji maombi sahihi, kujitambua, kujielewa, kutii Neno la MUNGU na kuenenda katika RO...
Comments
Post a Comment