MAMBO 10, TUNZA MUUJIZA WAKO
Mambo 10 ambayo yatatendeka kwako mwaka huu wa 2018.
Imeandikwa:-
Zaburi 20:8 “Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.”
1. Wote waliopanga mabaya juu yako watashuka chini nawe utachukua sehemu zao. Utachukua sehemu ya mtu aliyekuwa anataka kukushusha chini kwa jina la Yesu.
2. Kuna mashimo umechimbiwa 2017 Mungu atayafukia yote 2018 na hautayaona tena 2018. Kuna mtu alichimba shimo mahali ili utumbukie lakini Mungu amelifukia.
3. Kuna mtego wa mauti uliotegwa 2017 na mtego huo ukafichwa sana ili usiuone lakini 2018 Mungu ameufyatua mtego ule utamnasa aliyekutegea hautafyatuka bure lazima umnase aliyeutega kwa jina la Yesu.
Kifo siyo tukio bali ni roho inayoweza ikatumwa kwenda kwa mtu iutoe uhai wake. Kifo kinaweza kutumwa au kinaweza kutegwa mahali. Kwenye maandiko Imeandikwa:-
Ufunuo wa Yohana 6:8 “Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.”
2 Wafalme 4:40-41 “Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula. Lakini yeye akasema, Leteni unga. Naye akautupa ndani ya sufuria; akasema, Wapakulie watu, ili wale. Wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani.”
Kwenye kitabu cha wafalme utaona wanasema wana wa mfalme walikuwa wanakula chakula wakapiga kelele wakasema mauti imo sufuliani mtu wa Mungu akatupa unga mauti ikaondoka. Kwahiyo kifo siyo tukio bali kinaweza kutumwa kwako.
4. Utakuwa ni mwaka wa kicheko kwako, (utacheka mpaka watu watajua una meno mangapi). Lipo jambo litakalokuchekesha kwenye ndoa, biashara, masomo, nchi itacheka kila mtu atacheka. 2018 utakuwa ni mwaka wa kicheko kwako, utapata safari ya kwenda itakayokufanya uchekesha kwa jina la Yesu.
5. Kuna mtu amekunyima usingizi sana 2017 lakini 2018 utalala kama mtoto mchanga lakini yeye atakesha.
6. Kuna mtu utapata safari 2018 na hii safari itabadilisha maisha yako milele wala hutaukumbuka utumwa wako tena ila usimsahau Bwana aliyekupa utajiri.
7. Aliyekutesa 2017 Mungu amesema 2018 atapiga magoti mbele yako usimlipe kisasi mwache aende zake amejifunza Mungu wako anajibu kwa mvua na moto. Yule baba/mama aliyetoroka nyumbani kwako eti upendo umeisha utashangaa 2018 unapokea meseji anasema nimekumisi.
8. Kuna mtu umelia sana 2017 Mungu anasema 2018 amekupa kifua cha kuegama. Unalia kwenye ndoa, unalia kwenye kazi, unalia wizarani, Mungu amekupa kifua cha kuegama. (Tafasili ya kifua cha kuegama inategemea na mtu mwenyewe mwambie Mungu akupe tafsri ya kifua cha kuegama kwa jina la Yesu)
9. Uliumizwa sana 2017 ukawa unawaza mbona Mungu ameniacha? Mungu anasema aliruhusu ili ujifunze vita ndiyo maana amekuleta hapa, 2018 hutaona jeraha tena.
Kujenga kunahitaji fundi bali kubomoa hakuhitaji fundi, kujenga kunahitaji ramani lakini kubomoa hakuhitaji ramani, duniani waharibifu ni wengi kuliko wajenzi. Fimbo ya Musa iliyogawa bahari bado inatumika 2018 itatumika kugawa bahari yako kwa jina la Yesu.
10. LUKA 2:10 “MALAIKA AKAWAAMBIA, MSIOGOPE; KWA KUWA MIMI NINAWALETEA HABARI NJEMA YA FURAHA KUU ITAKAYOKUWA KWA WATU WOTE”
2018 ni mwaka wa habari njema itakayokuwa kwa watu wote lipo jambo litatendeka ambalo litakuwa furaha kuu kwa watanzania wote. Kuna watu wataalamu wa kuiwazia Tanzania mambo mabaya tu lakini sisi tunaiwazia mambo mema ambayo yatatokea kwa jina la Yesu. Mambo haya yakupate sawasawa na Imani yako kwa jina la Yesu.
Mambo ambayo mtumishi wa Mungu anaweza kufanya.
1. kwanza anayaona mambo kwenye ulimwengu wa roho anasema hii inaitwa.
2. Mtumishi wa Mungu anaweza na kuumba na kutengeneza jambo kwa kusema na ikawa unaposema nitakuwa salama sitapata ajali 2018 inakua vilevile kwasababu imeandikwa tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, Mungu alisema iwe nuru ikawa na sisi tukisema neno lolote inakua vilevile.
Bishop Dr.Josephat Gwajima
Comments
Post a Comment