BILLY GRAHAM AMELALA

BILLY GRAHAM
Billy Graham amepumzika akingoja ufufuo.

Sijamuona akitumia nguvu kusukuma watu waanguke.

Sijamuona akijiita nabii mkuu wa kizazi hiki ambaye matamko yote ya Kiroho yangetoka kwake.

Kama alivyomtegemea Yesu alitufundisha kumtegemea Yesu katika kila jambo.

Amen.

Mungu apumzishe ROHO yake katika usingizi Mwema hadi Yesu atakaporudi.

1 Wakorintho 15:12-26,35-38,42,46,48,51-54
[12]Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
[13]Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;
[14]tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.
[15]Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
[16]Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.
[17]Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.
[18]Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.
[19]Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.
[20]Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.
[21]Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.
[22]Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
[23]Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.
[24]Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
[25]Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
[26]Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
[35]Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?
[36]Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;
[37]nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;
[38]lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.
[42]Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika;
[46]Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho.
[48]Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.
[51]Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
[52]kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
[53]Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
[54]Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

VUNJA VIFUNGO

NJIA ZA KUMTIA MOYO MCHUNGAJI WAKO

MAMBO 10, TUNZA MUUJIZA WAKO